Ni picha nzuri ya kupendeza yenye nyota toka angani, iliyopigwa katika kituo cha kuangalia anga cha Ulaya ya Kusini! Lakini inaonekana kama kuna mtu amemwaga kitu katikati ya picha. Hivyo ndivyo mwanaanga wa kwanza aliyegundua doa la angani alivyofikiria. Ingawa maneno yake halisia yalikuwa kimashairi zaidi: alilifafanua kwa kusema “ni tone la wino katika anga ing’aayo”.
Tunachokiangalia katika picha hii ni mamilioni ya nyota zinazong’aa kutoka katika sehemu ya galaxi yetu ya Milky Way ing’aayo sana. Katika sehemu ya anga iliyojaa nyota katika picha ni vigumu sana kuona sehemu iliyo nyeusi. Ingawa katikati ya picha hiyo hiyo, karibu kabisa na nyota ing’aayo sana unaweza kuona wingu jeusi ambalo si la kawaida.
Unaweza kuona kama shimo lililowazi linaloikinga nyota, lakini shimo hili jeusi ni wingu dogo la vumbi lililojitenga mbele ya wigo wa nyota. Mawingu kama haya yanaitwa ‘Bok globules’. Yametengenezwa na chembe chembe ndogo za vumbi ambazo zinakinga miale ya nyota inayotoka nyuma yake na kufanya eneo hilo lionekane kama doa jeusi.
Bok globues ni masalia ya wingu kubwa linajulikanalo kama ‘molecular clouds’ au kwa jina rahisi ni ‘stellar nurseries’, kwa sababu nyota huzaliwa katika mawingu hayo makubwa! Karibu nyota milioni kumi zenye ukubwa sawa na Jua zinazaliwa katika wingu moja la molecular cloud! Nyota katika kundi linalowaka lililopo pichani zimetengenezwa kutoka katika wingu moja la molecular clouds, na Bok globule iliyopo karibu yake ni sehemu ndogo iliyobakia.
Dokezo
Baadhi ya madaktari wa akili huwapa wagonjwa wao mtihani wa kuvuja kwa wino katika karatasi ili kuangalia afya ya akili. Kutokana na umbo la wino uliovuja lililotengenezwa katika karatasi daktari huweza kugundua tabia za mgonjwa anapoliangalia. Je unaona nini kwenye doa jeusi? Naona mjusi. Je unafikiri hilo jibu lina maana kwetu!
Share: